REPOSITORY

UKIUSHI WA KANONI KATIKA HADITHI TEULE ZA WATOTO ZA JOHN KOBIA NA WADI WAMITILA

Show simple item record

dc.contributor.author MIRICHO, ERASTUS MUTAHI
dc.date.accessioned 2023-06-08T08:39:22Z
dc.date.available 2023-06-08T08:39:22Z
dc.date.issued 2021-03
dc.identifier.uri http://repository.laikipia.ac.ke/handle/123456789/363
dc.description.abstract Fasihi ya watoto inaweza kufasiliwa kama kazi ya sanaa inayotungwa ikilenga watoto kama hadhira kuu. Fasihi hii hutungwa na kuhakikiwa kwa misingi ya kanoni ambazo ni vigezo vya kupimia ubora wa fasihi hii. Vigezo hivi vinatokana ama na kazi ambazo zilifana sana kiasi cha kuigwa au na sifa za fasihi ya watoto zilizotolewa na wataalamu na ambazo imekuwa kama ni mwiko kuzikiuka. Hata hivyo, kumetokea waandishi wa hadithi za watoto wanaotunga kazi zilizokiuka kanoni ya fasihi hii kimaudhui na kifani. Maudhui ambayo yalichukuliwa kuwa yanafaa kushughulikiwa tu katika fasihi ya watu wazima, yanaanza kujipenyeza katika hadithi za watoto huku baadhi ya sifa za fani pia zikikiukwa. Kuna haja basi ya kuchunguza ni vipi ukiushi huu unavyojitokeza na kudhibitiwa ili hadithi ifungamane na tajriba ya watoto wanaolengwa. Madhumuni halisi ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza ukiushi wa kanoni ya maudhui katika hadithi teule za watoto za John Kobia na Wadi Wamitila; kuchanganua ukiushi wa kanoni ya fani katika hadithi teule za watoto za John Kobia na Wadi Wamitila na kutathmini mikakati ambayo waandishi wa hadithi teule wanatumia kudhibiti ukiushi wa kanoni. Utafiti huu ulitumia nadharia ya udenguzi ya Derrida (1976) na nadharia ya umitindo ya Leech (1969). Nadharia ya udenguzi ilitumiwa kutathminia ukiushi wa maudhui na fani. Utafiti huu uliongozwa na mihimili mikuu mitatu ya nadharia hii. Nadharia ya umitindo ilitumiwa kuchunguzia ukiushi wa fani na pia kutathminia mikakati ya kiubunifu aliyotumia mwandishi kudhibiti ukiushi. Mihimili mikuu mitatu ya nadharia ya umitindo iliongoza utafiti huu. Huu ulikuwa utafiti wa kimaelezo. Hadithi za watoto za waandishi hawa ziliteuliwa kimakusudi kwa kutumia sampuli lengwa kutokana na upekee wa kimaudhui na kifani uliodhihirisha ukiushi. Ilibainika wameandika hadithi kadhaa zenye ukiushi. Hadithi zilizoteuliwa zilisomwa kukusanya data kuhusu ukiushi wa kanoni kwa kujibu maswali ya utafiti. Data iliyopatikana kuhusu ukiushi wa kanoni katika kila hadithi ilichanganuliwa. Mwisho, matokeo na mapendekezo ya utafiti yaliwasilishwa kimaelezo. Matokeo yalibainisha kuwa hadithi zilizochunguzwa zilikiuka kanoni ya fasihi ya watoto kimaudhui na kifani lakini kwa njia iliyodhibitiwa. Utafiti huu unatarajiwa kuwa muhimu kwa wasomi na waandishi wa fasihi ya watoto. Unaongeza maarifa katika uhakiki wa hadithi za watoto kwa kuangazia mielekeo ya kimaudhui na kifani inayokiuka kanoni. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.publisher Laikipia University en_US
dc.subject MIRICHO ERASTUS MUTAHI en_US
dc.subject Laikipia University en_US
dc.title UKIUSHI WA KANONI KATIKA HADITHI TEULE ZA WATOTO ZA JOHN KOBIA NA WADI WAMITILA en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Browse

My Account