REPOSITORY

ULINGANISHI WA MAUMBO, MOTIFU NA CHANGAMOTO ZA MAJAGINA KATIKA TENDI ZA MIKIDADI NA MAYASA NA KALEVALA

Show simple item record

dc.contributor.author MWANGI, JACKSON NDUNG’U
dc.date.accessioned 2023-06-22T11:51:13Z
dc.date.available 2023-06-22T11:51:13Z
dc.date.issued 2021-07
dc.identifier.uri http://repository.laikipia.ac.ke/handle/123456789/408
dc.description.abstract Tendi za Kiswahili zimekuwepo katika maeneo ya Pwani ya Afrika Mashariki tangia karne ya 17 na zimekuwa zikienziwa, kudhaminiwa na kusawiri tamaduni na asasi z a wakazi hawa. Uwepo wa tendi katika maeneo ya Kiafrika uliwahi kuzua mjadala mkubwa kutoka kwa wasomi wa Kimagharibi waliodai kuwa Afrika hakuna tendi ila kinachodaiwa kuitwa tendi ni masimulizi ya kisifo tu. Wengine wamezifutilia mbali tendi hizi kwa kud ai kuwa maudhui yake ni ya kichawi na sihiri. Ukweli ni kwamba, utafiti uliofanywa na watafiti hawa uliegemea mitazamo ya Kimagharibi. Licha ya kuwa kuliibuka watafiti waliodai kuwa hakuna tofauti kati ya tendi za maeneo haya mawili, hakujafanywa utafiti l inganishi wa kutathmini ujitokezaji wa vipengele vya kimaumbo na motifu katika tendi za Kiswahili za Kiafrika na zile za Kimagharibi zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili. Madhumuni makuu yalikuwa ni kuhakiki maumbo yanayobainika baina ya tendi za Kiafrik a na zile za Kimagharibi. Mtafiti alinuia kuchunguza tendi mbili zinazopatikana katika maeneo ya Kiafrika na Kimagharibi. Tendi hizi ni Utendi wa Mikidadi na Mayasa unaopatikana Afrika na katika maeneo ya Kimagharibi Utendi wa Kalevala unaopatikana Finland . Mtafiti alichunguza tendi hizi mbili kutoka eneo la Afrika na Kimagharibi kwa sababu zina upekee katika mitindo na fani, zinabeba historia ya kipekee katika maeneo yao, zinaibua motifu mbalimbali na zinafungamana na madhumuni ya utafiti huu. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili kuu ambazo ni Nadharia ya Umtindo iliyoasisiwa na Barry na Nadharia ya Ruwaza ya Shujaa iliyoasisiwa na mwanafalsafa Joseph Campbell. Mihimili ya nadharia hizi ilitumiwa na mtafiti kueleza upeo na mipaka ya utafiti huu na pia ilisaidia kuchanganua data. Utafiti huu ulihusisha kusoma makala na kutumiwa kama data ya utafiti huu ambayo baadaye ilichanganuliwa na mwishowe kuelezea matokeo kwa kutumia mbinu ya kimaelezo. Utafiti huu pia ulihusisha ukusanyaji wa data moja kwa moja ku toka maktabani. Mahali pa utafiti palikuwa ni maktaba na sampuli ya utafiti huu ilikuwa Mayasa unaopatikana Afrika na Utendi wa Kalevala Utendi wa Mikidadi na unaopatikana maeneo ya Kimagharibi uliotafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Matokeo ya utafiti ya libaini kuwa vipengele vya kimaumbo, motifu na changamoto zinazowakumba majagina zilizobainika katika tendi za Kiafrika zilidhihirika pia katika tendi za Kimagharibi. Inatarajiwa kuwa utafiti huu utakuwa na mchango mkubwa kwa jamii ya wasomi hasa wanaoshu ghulikia fasihi linganishi na utajaribu kutatua ubishi ulioko kuhusu tendi za maeneo mbalimbali. Utafiti huu pia utasaidia kuhifadhi tendi za Kiswahili. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.publisher Laikipia University en_US
dc.subject Laikipia University en_US
dc.subject JACKSON NDUNG’U MWANGI en_US
dc.title ULINGANISHI WA MAUMBO, MOTIFU NA CHANGAMOTO ZA MAJAGINA KATIKA TENDI ZA MIKIDADI NA MAYASA NA KALEVALA en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Browse

My Account