REPOSITORY

DISKOSI YA MAFUNZO YA TENDO LA NDOA KATIKA JANDO MIONGONI MWA WAKIPSIGIS NCHINI KENYA

Show simple item record

dc.contributor.author KIMUTAI, KIRUI NICHOLAS
dc.date.accessioned 2025-04-08T08:35:27Z
dc.date.available 2025-04-08T08:35:27Z
dc.date.issued 2024-10-01
dc.identifier.uri http://repository.laikipia.ac.ke/handle/123456789/3580
dc.description.abstract Miviga za jandoni ni mojawapo ya tanzu za fasihi simulizi. Utanzu huu hutumiwa kupitisha mafunzo kuhusu masuala ya ngono kwa wavulana wakiwa jandoni. Mafunzo yanayohusu tendo la ndoa katika jamii yoyote huwa nyeti. Hata hivyo, hayazungumzwi hadharani. Yanapojitokeza katika kauli za wanajamii, huwasilishwa kwa mikakati mahususi ya kujaribu kuuficha uwazi huo. Ingawa wataalamu mbalimbali wamechunguza diskosi za tendo la ndoa katika nyanja tofauti tofauti, uchanganuzi wa diskosi za tendo la ndoa katika muktadha wa jandoni haujafanyiwa utafiti wa kina. Utafiti huu hivyo basi, ulidhamiria kuchanganua diskosi za tendo la ndoa zinavyojitokeza katika mafunzo ya jandoni katika jamii ya Wakipsigis. Malengo ya utafiti yalikuwa kuchanganua mada za diskosi za tendo la ndoa na kutathmini mikakati inayotumiwa katika mafunzo ya diskosi za tendo la ndoa katika shughuli za jando. Utafiti huu ulielekezwa na Nadharia ya Diskosi hasa kwa Mkabala wa Historia. Mihimili ya nadharia hii ni mikakati ya; urejelezi, uarifishaji, ubishi, mikabala, kuongeza na kufifisha makali ya usemi. Asilimia kubwa ya utafiti huu ilikuwa ya nyanjani, kwa ajili ya kukusanya data ya kimsingi. Aidha, mtafiti alihusisha utafiti wa maktabani ili kupata michango ya wataalamu wa awali kuhusu suala hili. Data ilikusanywa kwa njia ya mahojiano, kurekodi, picha na majadiliano. Jamii ya Wakipsigis ndio ilikuwa kundi lengwa la utafiti huu na mafunzo yanayohusu suala la tendo la ndoa jandoni yalilengwa. Data ya utafiti huu iliwasilishwa na kuchanganuliwa kwa kutumia mbinu ya kimaelezo ili kudadavua matokeo ya utafiti. Utafiti huu ulifanyika katika eneo la Bomet wanakoishi asilimia kubwa ya Wakipsigis. Ngariba watatu waliteuliwa kutoka maeneo matatu makuu ambayo ni Kaunti ndogo za Chepalungu, Bomet Mashariki na Sotik. Maeneo haya yaliteuliwa kwa kuwa yana utamaduni asilia ambao haujaathiriwa na tamaduni za kigeni na usasa. Sampuli ya utafiti huu ilihusisha kuteua watahiriwa wawili kutoka mfumo wa rika saba inayopatikana kwa jamii hiyo ili kupata data ya kutegemewa. Matokeo ya utafiti yameonyesha kwamba mada zinazozungumziwa ni; idhini ya kushiriki ngono, jinsi ya kushiriki tendo la ngono, washiriki katika tendo la ngono, unyeti na maadili katika tendo la ndoa. Baadhi ya mikakati inayotumiwa kupitisha mada hizi ni kama vile; jazanda, taashira, tasfida, sitiari, nyimbo na istihizai. Utafiti huu ulinuia kuongeza maarifa kwa wasomi, wahakiki na watafiti wa masuala ya uchanganuzi usemi. Matokeo ya utafiti huu yatafaa wataalamu wa lugha, wachanganuzi wa diskosi na utachangia kuelewa suala la diskosi katika muktadha wa jinsia. Aidha, utafiti huu utawaauni washikadau wote wanaohusika katika kubuni sera zinazohusiana na jinsia.. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.publisher LU en_US
dc.subject DISKOSI YA MAFUNZO YA TENDO LA NDOA en_US
dc.subject TENDO LA NDOA KATIKA JANDO MIONGONI MWA WAKIPSIGIS NCHINI KENYA en_US
dc.subject KIRUI NICHOLAS KIMUTAI en_US
dc.title DISKOSI YA MAFUNZO YA TENDO LA NDOA KATIKA JANDO MIONGONI MWA WAKIPSIGIS NCHINI KENYA en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Browse

My Account