REPOSITORY

ULINGANUZI WA USEMI WA KISIASA KATIKA KAMPENI ZA URAIS NCHINI KENYA MIEZI MITANO KABLA YA CHAGUZI ZA MWAKA WA 2007 NA 2013

Show simple item record

dc.contributor.author KARIITHI, FRANCIS M
dc.date.accessioned 2023-06-09T08:08:09Z
dc.date.available 2023-06-09T08:08:09Z
dc.date.issued 2015
dc.identifier.uri http://repository.laikipia.ac.ke/handle/123456789/399
dc.description.abstract Tangu maajilio ya vyama vingi vya kisiasa nchini Kenya lugha imekuwa ikitumiwa kama zana ya kisiasa na kijamii katika kukuza ushindani na kukolezea mikakati ya usemi wa kikabila ambao hunuiwa kutoa nafasi kwa mwanajamii kuyasimbua masuala fulani ya kijamii akilenga faida imrudie yeye. Kutokana na mabadiliko kadhaa ya kisheria ambayo yalitokea nchini Kenya baada ya uchaguzi wa 2007, haikuwa dhahiri ikiwa wanasiasa wangeusitiri usemi wao, kwa kuhofia kufunguliwa mashtaka endapo ingebainika kuwa usemi wao ungekuza chuki baina ya jamii mbalimbali nchini. Utafiti huu ulilinganua usemi wa wanasiasa miezi mitano kabla ya chaguzi za mwaka wa 2007 na 2013. Malengo ya utafiti huu yalikuwa kuzichunguza mada tofauti za usemi katika kampeni za urais nchini Kenya katika kipindi kilichokuwa chini ya utafiti huu. Utafiti huu vilevile ulijadili mikakati tofauti tofauti iliyotumiwa na wanasiasa katika kampeni za urais nchini Kenya; na kutathmini athari za usemi wa wanasiasa katika kampeni hizo. Nadharia ya Uchanganuzi Hakiki wa Usemi (UHU): Usemi – Mkabala wa Kihistoria (UMK) ilimwongoza mtafiti, ambapo mbinu ya maelezo ndiyo iliyotumiwa kuichanganulia data. Wanasiasa waliolengwa walikuwa Raila Odinga, Uhuru Kenyatta na William Ruto. Data ilikusanywa kwa njia ya kimakusudi (usampulishaji wa matukio kiuhakiki) kutoka kwenye magazeti ya The Daily Nation na The Standard ambamo nukuu za usemi wa wanasiasa hao za miezi mitano kabla ya chaguzi za mwaka 2007 na 2013 zilichanganuliwa. Mada za Usemi katika kampeni zilikuwa msingi wa uchanganuzi wa data husika. Ilibainika kuwa uteuzi wa mada za usemi huongozwa na masuala nyeti ya kihistoria katika jamii kama vile ardhi na masuala mengine ibuka. Aidha, ilibainika kuwa wanasiasa huiteua mikakati mbalimbali ambayo malengo yake huwa ni kuishawishi jamii; isitoshe, imedhihirika kwamba usemi huo wa kisiasa ulikuwa na athari kadhaa; kama vile, kujikariri kwa masuala ya kihistoria, kuzalika kwa miungano ya kikabila, kuibuka kwa usemi wa kitabaka, kuibuka kwa usemi wa kidini na kuchipuka kwa usemi wa kuumbuana miongoni mwa matukio mengine mengi. Utafiti huu umeonyesha kuwa lugha ni kiashiria cha masuala ya jamii na hivyo hali za kisiasa, hivyo basi, lugha inaweza kuonekana kama nguvu ya kuendeshea mabadiliko ya kisiasa na kijamii. Inatarajiwa kwamba utafiti huu ni mchango katika kuukuza uwanja wa uchanganuzi wa usemi wa kisiasa hasa ulinganuzi wa usemi wa kisiasa. Mwisho, inatarajiwa kuwa matokeo yatachangia katika kuyaelekeza mashirika mbalimbali ambayo yamepewa majukumu kuhakikisha kuwa uwajibikaji na utangamano unaafikiwa nchini kwa kubainisha pale mpaka wa ‘usemi wa chuki’ unaanzia na kuishia. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.publisher Laikipia University en_US
dc.subject SIASA en_US
dc.subject KAMPENI en_US
dc.subject CHAGUZI ZA MWAKA WA 2007 NA 2013 en_US
dc.title ULINGANUZI WA USEMI WA KISIASA KATIKA KAMPENI ZA URAIS NCHINI KENYA MIEZI MITANO KABLA YA CHAGUZI ZA MWAKA WA 2007 NA 2013 en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Browse

My Account